5/16/2018

Tatizo la Vidonda Mdomoni

Vidonda mdomoni  husababisha sana maumivu makali  pamoja na kumfanya mtu asiweze kuongea vizuri na watu.Vidonda hivi  husababishwa na kutafuta kwa muda mrefu hasa bigijii au kitu chochote,  uvutaji wa sigara,maambukizi ya virusi, bakteria na fungasi sambamba na ukosefu wa madini   na virutubisho vya folic, zinc, vitamin c,vitamin B12, na madini ya chuma.

Vidonda hivi huwaathiri sana watu wengi na hutokea sana kwenye lips, ulimi , mashavu,  kingo na kuta za meno ambapo pia huweza kusambaa hadi kwenye koromeo endapo havitatibiwa mapema.


Pamoja na kutembelea hospitali ambapo dawa kama za antibiotiki, fangasi, virusi na zile za kupunguza maumivu na uvimbe huweza kutolewa kulingana na ukubwa wa tatzo pia unaweza kufanya yafuatayo kujitibu nyumbani


  • Epuka vyakula na vinywaji vya moto au baridi sana kwani huchelewesha kupona kwa vidonda
  • Kunywa juice ya matunda mbali mbali itakayokuwezesha kupata virutubisho na madini ambayo huongeza kinga ya mwili
  • Kunywa maji mengi kila siku ambayo sio ya moto wala baridi
  • Piga mswaki mara kwa mara na taratibu ili kuepuka kukwangua na kutonesha sehemu zenye vidonda
  • Kula sana matunda asa machungwa, machenza na malimao kwani yana kiasi kikubwa cha vitamin ambayo huongeza kinga ya mwili. Pia yana asidi ambayo inaweza kuua wadudu wanaokuwepo mdomoni
  • Unaweza kununua pia Maltivitamini dawa yenye mchanganyiko wa virutubisho vingi ambavyo huweza kusaidia kurudisha kinga ya mwili katika hali ya kawaida
  • Kama vidonda vinaambatana na maumivu makali tumia dawa ya kutuliza maumivu au kuweka barafu ambayo hupunguza maumivu kwa muda
  • Tumia Asali ambayo husaidi kuua vimelea, kuponya makovu na kulainisha sehemu zenye vidonda
  • Kunywa maji ya nazi(madafu) ambayo upoza mwili na huua wadudu hatari mdomoni sambamba na kupaka mafuta ya nazi kwenye kidonda ili kupona haraka.


Kumbuka vidonda visivyopona kwa muda zaidi ya wiki mbili vinaweza kuashiria tatizo kubwa na sugu mwilini hivyo inakupasa kufika hospitali ambapo utapewa dawa za bakteria, fungasi, virusi au dawa nyingine zozote kulinga na ukubwa na visababishi vya tatizo.