https://monetag.com/?ref_id=TTIb Boko Haram yafanya shambulizi na kuua wanne | Muungwana BLOG

Boko Haram yafanya shambulizi na kuua wanne


Watu wanne wameripotiwa kupoteza maisha katika shambulizi la Boko Haramu nchini Nigeria. Shambulizi hilo limetokea kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Kamanda wa polisi wa eneo hilo  Damian Chukwu amesema kuwa magaidi hao walivamia kijiji na kuanza kumimina risasi kwa raia.

Idadi kubwa ya wananchi wamejeruhiwa katika shambulizi hilo. Nigeria imekuwa ikiandamwa na mashambulizi ya boko haramu mara kwa mara.