Dk Bashiru atishia kufukuza wanachama wenye makundi CCM


Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ameweka bayana kwamba atawafukuza uanachama watendaji wote watakaoonekana kushabikia makundi ya siasa ndani ya chama hicho.

Leo katika makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma  Dk. Bashiru ameyasema wakati akizungumza na wanachama pamoja na watumishi wa chama hicho mkoani huko ambapo ameweka wazi kuwa makundi hayajengi.

Dk Bashiru amesema ni marufuku watendaji wa chama hicho kuwa na makundi ya siasa ndani kwani hali hiyo ikitokea chama hakiwezi kuendelea mbele.

“Ni marufuku mtendaji wa chama kumshangilia mgombea wa kisiasa, kwani hiyo inapelekea kuwa na makundi, sasa tujiulize kila mtendaji akiwa na mgombea wake chama kitakalika? Nitawafukuza watendaji wote ambao wataonekana wanabeba mikoba wa wagombea, waacheni wanachama wa kawaida wafanye hivyo ila si ninyi watendaji ambao mnalipwa hela za wananchama,” amesema.