Israel yakamata mateka wapalestina 10 wakiwemo wanahabari


Jeshi la Israel limewakamata wapalestina 10 wakiwemo waandishi wa habari katika maandamano ya amani ya kupinga  kupokonywa kwa ardhi Kusini mwa Ukingo wa Magharibi.

Waandishi wawili wa habari pia wamekamatwa na jeshi la Israel.

Maandamano hayo yamefanyika katika eneo la Bani Naim, Mashariki mwa Hebron. jeshi la Israel limefahamisha kufunga eneo hilo.

Mashhour Wahwah  na Azmi Banat ndio waandishi wa habari waliokamatwa na jeshi la Israel.