Mbowe adondoka ghafla, akimbizwa Muhimbili


Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe leo Juni 18 amepata tatizo la kiafya ambalo limepelekea kudondoka ghafla leo alfajili na kukimbizwa hospitalia ya Taifa ya Muhimbili na kuwekwa kitengo cha huduma ya dharura.

Akizungumza na Muungwana blog msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo mpaka sasa Mbowe yupo Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Tukio hilo limejili wakati Mwenyekiti huyo akikabiliwa na kesi ambapo alitakiwa kufika Mahakama ya Kisutu leo kujibu kesi inayomkabili ikiwa yeye ni mshitakiwa namba moja.