Mwenyekiti wa Chadema avamiwa na kuporwa fedha



Na Timothy Itembe Tarime,
MWENYEKITI wa mtaa wa Bugosi kata ya Turuwa ndani ya halmashauri ya Mji wa Tarime mkioani Mara,Zacharia Chacha Ghati (CHADEMA) juzi majira ya saa 04 usiku alivamiwa na kundi la watu sita wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati njiani akielekea Nyumbani kwake

Kundi hilo la Watu  walimvamia na kumpiga  pamoja na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili wake wakati ambapo walimteka huku wakimpiga kwa kutumia  silaha mbalimbali za jadi marungu,mapanga mishale pamoja na nondo hadi kusababisha kupelekwas kualzwa katika hospitali ya Wilaya inayomilikiwa na halmashauri ya Mji wa Tarime.

Akionglelea tukio hilo,Bashiri Abdala jina maarufu Sauti ambaye ni  diwani kata ya Nyamisangura pia makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Tarime alisema kuwa tukio hilo halihuisiani na maswala ya kisiasa isipokuwa ni tukio la kiujambazi.

Sauti alitumia nafasi hiyo kulitaka jaeshi la polisi mkoa wa kipolisiTarime Na Rorya  kutumia taaluma yao kukomesha vitendo vya kuhalifu pamoja na kuwahi eneo la tukiop pindi wanapokuwa wamepewa taarifa na wananchi kuwa kuna tukio la kuihalifu ili kukabiliana na majambazi.

Sauti ametumia nafasi hiyo pia kuwataka wanachi na jamii kwa ujumla kutoa taarifa sehemu husika pindi wanapokuwa wanamashaka na makundi ambayo wanayahisi kuwa niyakiuhalifu pamoja na kuongeza kuwa hali ya majeruhi huyo inaendelea vizuri.

"Tukio la kuvamiwa mwenyekiti wangu was mtaa wa  Bugosi alihusiani na maswala ya kisiasa isipokua ni tukio la kiujambazi natumia nafasi hii kulitaka jeshi la polisi mkoa wa kipolis Tarime/Rorya kuacha visingizio vya kusema kuwa hawana mafuta,kwenye magari wako mbali na tukio magari yameharibika pale ambapo kuna tukio linapokuwa limetokea na wananchi wakawa wametoa taarifa ili kuomba masaada"alisema Sauti.

Akiwa anapati matibabu wodini namba Tatu ya wanaume ndani ya hospitali ya wilaya inayomilikiwa na halmashauri ya Mji wa TYarime mwenyekiti huyo,Zacharia Chacha Gahati  alisema kuwa alivamiwa majira ya saa 04 usiku wakati alipokuwa njiani akitoka  kumsindikiza rafiki yake sherehe huku Bisalwi ambapo majambazi hao walimvamia na kumpiga huku wakimjeruhi sehemu mbalimbami za mwili pamoja na kumpora shilingi laki tatu na alfu ishirini.

"Nikiwa njiani baada ya kuachana na rafiki yangu ambaye nilikuwa nimempeleka ugeni wa kumchinjia Mama mkwe wake Bisalwi nilivamiwa na kundi la watu sita ambao wanadhaniwa kuwa majambazi na kunipiga sehemu mbaimbali za mwili wangu huku wakiwa na silaha za jadi ikiwemo nondo wamenipiga mgongono,magotini,kichwani na machoni pamoja na kunipora shilingi 300,000"alisema Ghati.

Kwa upasnde wake kamanda mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya,Henry Mwaibambe aliwaambia waandhishi wa habari kuwa tukio hilo hajalipata ofisini kwake na kuwa anafuatilia ili kujua na atakapolipata atatoa taarifa kwa waandishi wa habari.