https://monetag.com/?ref_id=TTIb Nadal agomea mashindano ya Uingereza | Muungwana BLOG

Nadal agomea mashindano ya Uingereza


Mcheza Tenisi namba moja duniani Mhispania Rafael Nadal, amejitoa kwenye michuano ya tenisi ya (Fever-Tree Championships) inayotarajiwa kufanyika kwenye klabu ya Malkia jijini London Uingereza.

Nadal ambaye ameshinda taji lake la 11 la Michuano ya wazi ya Ufaransa Jumapili iliyopita, amesema sababu kuu ya kujitoa kwenye michuano hiyo ni kupata muda wa kujiandaa na michuano ya Wimbledon inayoanza Julai 2.

"Nimeongea na madaktari wangu wamenishauri nipumzike ili niweze kuweka sawa mwili wangu kabla ya kuingia kwenye michuano ya Wimbledon'', amesema Nadal mwenye miaka 32.

Aidha Nadal amewaomba msamaha mashabiki wake pamoja na waandaaji wa michuano hiyo ambao walikuwa wamejiandaa kumuona nguli huyo wa tenisi duniani.