6/13/2018

Navy Kenzo kumwaga mkwanja kwa mashabiki wao


Kundi la muziki Bongo, Navy Kenzo limetangaza fursa kwa vijana au mashabiki wao.

Guess what, fursa hii ni kwa wale wanaojua kucheza ambapo watatuma clip wakicheza wimbo mpya wa kundi hilo uitwao Fella.

Ambaye ataibuka mshindi atajinyakulia dola za kimarekani 1,000 zaidi ya Tsh. 2,200,000.

Fella ni wimbo wa kwanza kwa Navy Kenzo kutoa mwaka huu tangu pale walipomshirikisha Patoranking katika wimbo wao unaokwenda kwa jina la Bajaj uliotoka June 19, 2017.