6/13/2018

Polisi Tanga yapiga marufuku disko toto siku ya Eid


Wakati zikiwa zimebaki siku chache kuelekea Sikukuu ya Eid al Fitri ambayo hufanyika baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani, Jeshi la polisi mkoani Tanga limepiga marufuku disko toto kwenye kumbi za starehe mkoani humo,

Hayo yamesemwa na kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Kamishina Msaidizi Edward Bukombe  wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake.

Hata hivyo kamanda huyo akatoa angalizo kwa wageni kutoka nje ya mji wa tanga kuwa ni marufuku kuogelea maeneo ya bahari yasio rasmi.

Tamko hilo la jeshi la polisi limekuja baada ya kipindi kama hiki cha sikukuu za Eid kwa mwaka jana baadhi ya watoto kujeruhiwa kutokana na msongamano uliotokea kwenye baadhi ya kumbi za starehe wilayani Handeni.