6/13/2018

Shemeji yake Diamond awawakia wanaomponda mkewe


MENEJA wa wanamuziki mbalimbali Bongo, Hamad Manungwa ‘Petit Man’ amewakia madai ya kwamba mkewe Asma Khan ‘Esma Platnumz’ hajui kupika na kuweka wazi kuwa, wanaosema hivyo wana lao jambo.

Petit Man alifikia hatua ya kusema hayo baada ya hivi karibuni kutupia video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikionesha futari ambayo ilionekana kutopikwa vizuri na watu kuanza kumshambulia kuwa mkewe hajui kupika.

“Unajua mimi sibishani hata siku moja na watu wa mitandaoni kwa sababu najua wazi sio mke wangu aliyepika ile futari. Akipika yeye chakula kinakuwa cha uhakika, nikila nasikia raha hadi najivunia kumuoa, hao wanaosema Esma hajui kupika, wana lao jambo,” alisema Petit Man