https://monetag.com/?ref_id=TTIb Timu zapania kupata pointi nyingi kwenye Bball Kings | Muungwana BLOG

Timu zapania kupata pointi nyingi kwenye Bball Kings


Baadhi ya timu  ambazo zilishiriki hatua ya 16 bora ya mashindano ya mpira wa Kikapu Sprite Bball Kings mwaka jana, na zile zilizoishia hatua ya mchujo zimepania mwaka huu kuhakikisha zinakusanya pointi nyingi ili ziende 16 bora na hatimaye kupigania ubingwa.

Wakiongea na eatv.tv kwa nyakati tofauti wawakilishi wa timu hizo, wamesema mwaka jana walikuwa wageni wa mashindano hivyo mwaka huu wamefanya maandalizi mazuri ambayo hawaoni namna ya kuishia hatua za awali.

Kocha wa timu ya Flying Dribblers, Geoffrey Lea amesema timu yake ilitolewa mwaka jana ambapo yeye alikuwa mchezaji lakini msimu huu ameamua kukaa kwenye benchi la ufundi na anaamini ataifundisha vizuri timu yake na itaibuka mabingwa.

Naye Jovi Charles wa Dream Chaser amesema msimu huu wameshapata uzoefu na hawana cha kupoteza maana wameshaanza maandalizi muda mrefu na watahakikisha wanapata pointi nyingi kwenye mechi yao ya mchujo ili waweze kusonga mbele zaidi.

Kwenye droo iliyofanyika Juni 20, 2018, Flying Dribblers imepangwa kucheza mechi yake ya mchujo dhidi ya Kurasini Worriors wakati Dream Chaser watakipiga na TMK Heroes. Baada ya mechi 25 za mchujo washindi 15 wenye pointi nyingi wataungana na Mchenga Bball Stars kwenye hatua ya 16 bora.