Ulega aendelea na ziara asikiliza kero za wananchi


MBUNGE wa Mkuranga na Naibu waziri mwenye dhamana katika sekta ya Ufugaji na Uvuvi Abdallah ulega ameendelea na ziara yake katika jimbo la Mkuranga katika kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi.

Ulega amesisitiza umoja na ushikamano  katika kuleta maendeleo katika jimbo hilo kwa mustakabali wa kizazi kijacho na amesema kuwa  anatambua changamoto ambazo bado zinazikabili jimbo lao na ataendelea kupambana nazo.


Ulega amefafanua kuwa kuwa, kuhusu maeneo yenye changamoto kama  miundombinu ya barabara kukatika baada ya mvua kupita tayari fedha zimetengwa kwa  maeneo hayo na kinachosubiriwa ni utekelezaji wa makandarasi.

Ulega amesisitiza kuwa ataendelea na jitihada zake na kushirikiana na wadau wa maendeleo katika  kupunguza kama sio kumaliza kero ambazo bado zipo katika baadhi ya maeneo hasa katika  elimu, afya na masuala ya kijamii.


Yasin Ligwema mkazi wa Mkuranga ameeleza kuwa vyoo vipewe vipaumbele sana katika shule ili kuwaweka wanafunzi hasa watoto wa kike katika kujisitiri, aidha wananchi  wamempongeza Mbunge wao katika kutoa vipaumbele katika masuala ya maji, elimu na afya.

Ulega alihitimisha ziara hiyo kukabidhi zakatulfitry kwa wajumbe waliohudhuria.