Uturuki wameanza kupiga kura kumchagua Rais na Wabunge


Raia wa Uturuki wameanza kupiga kura kumchagua rais mpya na wabunge watakao wakilisha majimbo yao.

Watu 56 322 632  wamejiandikisha kupiga kura kumchagua rais mpya miongoni mwa wagombea kutoka katika vyama tofauti nchini Uturuki.

Waturuki wanoaishi ugenini wamepewa fursa ya kuchagua hadi  jioni ya leo. Waturuki wanaoishi nchini Uturuki wameanza zoezi hilo la upigaji kura.