https://monetag.com/?ref_id=TTIb Baada ya maandamano kufanyika Uganda kupitia upya sheria ya mitandao | Muungwana BLOG

Baada ya maandamano kufanyika Uganda kupitia upya sheria ya mitandao


Serikali ya Uganda imetangaza kwamba tozo la kodi ya mitandao ya kijamii huduma ya kutuma pesa kwa simu itaangaliwa upya.

Kodi hiyo ya shilingi 200 za Uganda ambayo ni sawa na $0.05 inayotozwa ili mtu aweze kutumia mitandao kama Twitter na Facebook imechangia kuzuka maandamano nchini.

Lakini hakuna hakikisho kuwa kodi hiyo itaondolewa na huenda ikachukua wiki kadhaa kabla ya kuidhinishwa mageuzi yoyote yale.

Baadhi ya wabunge wanashinikiza kodi hiyo isitishwe kwa muda. Bunge litajadili hatua inayofuata kesho.

Mapema leo Jumatano Polisi nchini imefyetua gesi ya kutoa machozi na risasi hewani kutawanya kundi la waandamanji wanaopinga kodi iliyoidhinishwa ya kutumia mitandao ya kijamii.

Mwandishi wa BBC anasema polisi wamejaribu kumkamata mbunge ambaye pia ni muimbaji mashuhuri Robert Kyagulany, anayefahamika kwa umaarufu Bobi Wine, aliyeongoza maandamano hayo, lakini amefanikiwa kutoroka.

Mpiga picha mmoja katika maandamano hayo amekuwa akituma picha katika mtandao wa kijamii Twitter kuhusu yanayoendelea:

Kodi hiyo iliyoidhinishwa mwanzoni mwa mweiz huu inahitaji watumiaji mitandao ya kijamii nchini kulipa shilingi 200 za Uganda [$0.05, £0.04] ili waweze kutumia mitandao kama Facebook, Twitter na WhatsApp.


Bunge liliidhinisha kodi hiyo mnamo Mei baada ya rais Yoweri Museveni kushinikiza mageuzi hayo.

Rais Museveni a anaoutaja kuwa maoni, upendeleo, matusi na hata chati kwa marafiki.

Katika barua aliyomuandikia waziri wa fedha mnamo Machi, rais Museveni amesema kodi kwa mitandao ya kijamii inaweza kuongeza kipato cha serikali, na kupunguza mikopo inayochukua serikali na pesa za ufadhili.

Ameongeza kwamba haungi mkono kodi iitozwe kwa matumizi jumla ya mtandao kwasababu hili litaathiri matumizi yake kwa misingi ya 'elimu, na utafiti '.

Waziri wa habari na mawasiliano Uganda Frank Tumwebaze pia ametetea kuidhinishwa kwa kodi hiyo, akisema kwamba fedha zitakazopatikana zitatumiwa 'kuwekeza katika rasilmali zaidi za kimitandao'