CCM, Chadema wapigana vikumbo Babati


Na John Walter Babati
Chama cha Mapinduzi CCM kimesema kuwa kitaibuka na ushindi mkubwa kwenye uchaguzi mdogo wa marudio udiwani katika kata ya Bagara jimbo la Babati mjini.

Hayo yamesemwa na Katibu wa chama hicho Babati mjini  Faisal Hamad  ambapo amesema kuwa Chama hicho hakina hofu ya ushindi.

Amesema kuwa CCM kimefanya maandalizi makubwa hivyo kwao ushindi ni lazima katika kata ya Bagara inayorudia uchaguzi.

Wakati CCM wakizungumza hayo Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Zahr Mussa amesema kuwa wananchi ndio watakao amua nani wa kumpa kura.

Hata hivyo, amewataka wapiga kura kufuata taratibu zote zilizowekwa ili kuondokana na usumbufu ambao unaweza kujitokeza na kwamba wamejipanga kulinda kura.

Uchaguzi huo wa marudio katika kata ya Bagara Babati mjini unakuja baada ya aliekuwa diwani wa kata hiyo kupitia chama Cha Demokrasia na Maendeo Chadema Bonifasi Nikodemu kuhama chama hicho na kuelekea Chama cha Mapinduzi kwa madai ya kuunga mkono jitihada zinzaofanywa na Rais Magufuli.

Mgombea kwa tiketi ya Chadema ni  Mathias Zebedayo ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa Miomboni wakati kwa upande wa Ccm aliyetoka Chadema Bwana Nyeusi ndie aliepata nafasi ya kugombea kupitia tikiet ya Chama cha Mapinduzi.