7/11/2018

RCO atoa ushahidi kwenye kesi ya Halima Mdee


MKUU wa Upelelezi Wilaya ya Ilala (RCO), Davis Msangi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa hajawahi kumuhoji Rais John Magufuli jinsi anavyojisikia kuhusu maneno yaliyotamkwa na mbunge wa Kawe Halima Mdee dhidi yake.

RCO Msangi ameyaeleza hayo leo mahakamani hapo wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alipokuwa akijibu swali la Wakili wa utetezi Peter Kibatala.

Katika kesi hiyo, Mdee anakabiliwa na shtaka la kutoa lugha chafu kwa Rais Dk. John Magufuli.

Akimuhoji shahidi huyo,Wakili Kibatala alimuuliza Msangi kama anamfahamu Rais John Magufuli na anaishi wapi. alijibu kuwa anaishi Ikulu. Pia alimuuliza shahidi huyo kama aliwahi kwenda kumuhoji jinsi anavyojisikia kuhusu maneno yanayodaiwa kutamkwa na Mdee kwa sababu yeye ndiyo muhanga.

RCO Msangi alijibu kuwa hajawahi kwenda kumuhoji wala hakutumia taratibu zozote za kumuhoji.

RCO Msangi katika ushahidi wake amedai kuwa hafahamu msimamo wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana na kauli ya Rais Magufuli kuhusu watoto wa kike waliopata mimba shule wasirud