Wakimbizi 30,000 warejea nchini Burundi


Zaidi ya wakimbizi 30,000 wa Burundi wamerudi nyumbani kutoka kwa kambi zao nchini Tanzania tangu mpango wa wakimbizi hao kurudi nyumbani kwa hiari uanze mapema mwaka huu.

Hatua hii inakuja baada ya mkutano kati ya Rais wa Tanzania John Magufuli na mwenzake rais wa Burundi Pierre Nkurunziza mwezi Julai mwaka uliopita, wakati waliwashauri wakimbzi hao kurudi kwao.

Wito huo mara moja ulianza kukosolewa kutoka kwa makundi wa kutetea haki kwa sababu bado kuna ripoti za ukiukaji wa haki za binadamu nchini Burundi.

Zaidi ya watu 310,000 raia wa Burundi walikimbia nchi yao mwaka 2015 baada ya Burundi kutumbukia kwenye mzozo wakati Rais Pierre Nkurunziza, alishinda uchaguzi kwenye muhula wa tatu uliokumbwa na utata na ambao ulisababisha kuzuka ghasia nchini humo.