7/11/2018

Wanafunzi wa kike wapata msaada wa taulo


Wadau wa elimu  kutoka Taasisi binafsi wametoa taulo zenye uwezo wa  kufuliwa na kutumika kwa zaidi ya moja kwa  wanafunzi wa kike  kutoka jamii ya kifugaji kwa shule nane za wilaya ya Longido.

Wakizungumza katika zoezi la ugawaji wa taulo hizo wadau wanasema wamefikia hatua hiyo kwa lengo la kuboresha mahuzurio ya wanafunzi wa kike ambao wengi wao ushindwa  kuhudhuria masomo mara kadhaa kwa mwezi baada ya kukosa kinga hizo.

Mbunge wa Longido Dk Steven Kiruswa anasema msaada huo umekuja kwa wakati ukilinganisha na hali halisi ya maeneo hayo na Mkurugenzi wa halmshauri ya Longido Jumaa Mhina anasema msaada huo utasaidia kuwarudisha wanafunzi wa kike kwenye mstari wa mahudhurio ya masomo yao.

Baadhi ya wanafunzi wanasema wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la ukosefu wa taulo hivyo wameomba wadau wengine kujitokeza kuwasaidia.