AY apata mtoto wa kiume

 Mke wa msanii mkongwe wa muziki wa hip hop, Ambwene Yessayah aka AY aitwaye, Remy siku ya jana amejifungua mtoto wa kwanza wa kiume huko Dallas -Texas nchini Marekani.

Jumatatu hii rapa huyo ameutaarifu umma kwamba mke wake huyo amepata mtoto wa kiume aitwaye Aviel ikiwa ni miezi 6 toka wawili hao waingie kwenye maisha ya ndoa.

“Mungu ni mwema na namshukuru sana kwa kutubariki mimi na My Beautiful Wife #Remy tarehe 12.08.2018 Medical City Healthcare Dallas -Texas tumepata mtoto wa kiume AVIEL maana yake GOD IS MY FATHER…. 3.9Kgs & 27 inches…Welcome to the World AVIEL YESSAYAH 🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿,” aliandika rapa huyo kupitia instagram yake.

Mke wa rapa huyo ana asili ya Rwanda.