8/10/2018

Kauli ya TFF baada ya Polisi kumpiga Mwandishi wa Habari

 Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) limedai kuwa limesikitishwa na kitendo cha Jeshi la Polisi  Agosti 8, 2018 kumpiga Mwandishi wa Habari za michezo akiwa uwanjani kwenye mechi ya kirafiki kati ya Simba dhidi ya Asante Kotoko.

Taarifa ya kulaani tukio hilo imetolewa na Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo ambaye amesema kuwa watafuatilia kila kitu ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.