Man City yatwaa Ngao ya Jamii ikiichapa Chelsea


Kocha mpya wa Chelsea, Maurizio Sarri ameanza vibaya kibarua chake cha kuinoa timu hiyo baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Manchester City inayonolewa na Pep Guardiola.

Mchezo huo ni wa ngao ya jamii na uhusisha bingwa wa Ligi kuu ya England ambaye ni Man City na bingwa wa Kombe la FA ambaye ni Chelsea.

Magoli yaliyoipa ubingwa wa taji hilo yamefungwa na Mshambuliaji Sergio Kun Aguero dakika ya 13, 58 ya mchezo huo.

Pazia rasmi la Ligi kuu ya England linatarajia kufunguliwa rasmi Ijumaa ya wiki inayoanza kesho.