Moyes akaribia kupata shavu la kuinoa Marekani


Kiungo wa Wolves Mreno Ruben Neves mwenye miaka 21 ameingia kwenye rada za Manchester City na klabu hiyo inataka kumsajili mchezaji huyo katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari kwa dau la pauni milioni 60(Sun on Sunday)

Klabu ya Barcelona imekubali kuwa timu ya Manchester United haitomuuza kiungo wake Mfaransa Paul Pogba, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili tarehe 31, mwezi huu, ila wataangalia uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo dirisha lijalo la usajili . (Sunday Express)

Bosi wa zamani wa vilabu vya Everton, Manchester United, Sunderland na West Ham David Moyes anaongoza mbio za kupewa nafasi ya kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Marekani (Sunday Times - subscription only

Manchester City wameambiwa watalazimika kuilipa Borussia Dortmund's kiasi cha pauni milioni 68, kama inataka kumsajili kiungo Julian Weigl, ambae pia anawindwa na miamba ya soka ya Ufaransa Paris St-Germain (France Football, via Sun on Sunday)

Chelsea iko tayari kusikiliza ofa itayokuja klabuni hapo ikimtaka mchezaji wa kiungo Danny Drinkwater, ambae ameanza katika michezo mitano tu ya msimu uliopita akiwa amesajiliwa kwa kiasi cha pauni 35 akitokea Leicester City (Mail on Sunday)

Meneja wa Newcastle, Rafael Benitez anawaniwa na klabu ya Tianjin Quanjian,ya nchini china inayoshiriki katika ligi ya nchi hiyo (Sunday Mirror)

Tottenham inatarajia kuweka kiasi cha pauni milioni 10 mwezi Januari ili kupata saini ya beki kinda wa Celtic Kieran Tierney, mwenye miaka 21.(Sunday Express)

Meneja wa Aston Villa, Steve Bruce, anataka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham mpaka mwishoni mwa msimu (Birmingham Mail)

Liverpool inajianda kumuongezea mshahara beki wake Andrew Robertson, baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika msimu wake wa kwanza (Sunday Mirror