Mwili wa Savimbi kufukuliwa ili uzikwe kwa heshima


Mwili wa aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Angola Jonas Savimbi kufukuliwa kabla ya mwisho wa mwaka huu ili upate kupewa maziko mazuri, kwa mujibu wa chama chake cha Unita kilichonukuliwa na shirika la habari la AFP.

Kiongozi wa sasa wa chama cha Unita Isaias Samakuva, alitangaza kuwa mwili wa Savimbia utafukuliwa baada ya kukutana na rais Joao Lourenco kwenye mji mkuu Luanda siku ya Jumatano.

Savimbi aliuawa na vikosi vya serikali tarehe 22 Februari mwaka 2002 na kuzikwa siku iliyofuatia kwenye mkoa uliopo Mashariki wa Mexico.

Wiki sita baadaye Unita walisaini makubaliana ya amani na serikali na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 27.