Profesa Lipumba atinga Zanzibar, afunguka kuhusu uchaguzi 2020


Na Thabit Madai, Zanzibar
Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof. Ibrahimu Lipumba amesema chama chicho kipo tayari kushiriki katika uchaguzi mdogo wa uwakilishi katika jimbo la Jangombe.

Akizungumza na Wanachama pamoja na viongozi wa CUF wanaomuunga mkono kwa upande wa Zanzibar Prof Lipumba amesema hawawezi kuendelea na siasa za kususia chaguzi mbalimbali zinazoendelea nchini hivyo wanachama wajipange kuweza kushiriki katika uchaguzi mdogo wa marejeo katika jimbo la Jangombe.

“Kamwe hatuwezi kila siku kuacha kushiriki katika uchaguzi wowote jambo ambalo linapelekea kushusha imani na hadhi ya chama chetu” alisema Prof. Lipumba.

Aidha prof Lipumba amesema kuwa chama cha CUF    kinauwezo kubwa wa kushinda  uchanguzi  ujao  wa mwaka 2020 endapo viongozi  na wafuasi wa chama hicho  watashirikiana  katika kukijenga chama na kuondoa matabaka yanayochangia kukiyumbisha chama hicho wakati huu.

Amesema 2020 CUF watashiriki  uchaguzi kwa kusimamisha viongozi kwa ngazi zote Urais, Ubunge, Udiwani na Uwakilishi  ili kuweza kuwapa haki yao ya kikatiba na kuweza kusimamia na kulinda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Hata hivyo Amesema chama cha wananchi Cuf kitaendelea kuunga mkono Upatikanaji wa serikali ya Umoja Wa kitaifa na muungano wa serikali ya TATU.

Amesema chama cha CUF kwa upande wa bara kipo vizuri hivyo nguvu zinahitajika kwa upande wa Zanzibar hivyo Maalim Seif kwa nafasi yake anayo nafasi kubwa kuhamasisha wafuasi wa chama hicho kutovunjiaka moyo na kuendelea kukiunga mkono chama na kusimama imara.

Prof. Lipumba amemtaka maalim seif sharif hamadi kujirudi na kuacha kuendelea na siasa zisizokuwa na tija kwa taifa badala yake ajirudi na kuendeleza chama kwa msingi iliyowekwa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya mjini amesema imefika wakati cuf ikatae siasa za ubaguzi ambazo hazina faida yoyote kwa taifa.

"Tumechoka kubaguliwa huyu mbara , huyu mzanzibar, huyu mpemba na huyu muunguja" alisema mwenyekiti huyo wa cuf wilaya ya mjini unguja.

Mkutano huo wa viongozi na wanachama umefanyika katika ukumbi wa  wananchi  chama chawananchi CUF  beit-lyamini bwawani mjini unguja.