Rais asaini sheria mpya ya kubana mitandao


Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amesaini mkataba mpya ambao unawabana watu kutumia mtandao kwa kiwango kikubwa.

Sheria hii ya mtandao inamaanisha kwamba tovuti zinaweza kuzuiwa nchini humo ikiwa zinaonekana kuwa tishio kwa usalama wa taifa hilo au uchumi wake.

Mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kuendesha, au kutembelea, tovuti za aina hiyo anaweza kufungwa au kulipishwa faini.

Mamlaka imesema kwamba hatua mpya zitahitajikia ili kukabiliana na ugaidi na vurugu za aina yeyote.

Makundi ya kutetea haki za binadamu zimeishutumu serikali kwa kujaribu kuwanyima haki wapinzani.

Taasisi iliyopo Cairo inayoangazia uhuru wa kufikiri na kujieleza 'Association of Freedom of Thought and Expression' imesema zaidi ya tovuti 500 zimefungiwa mpaka sasa nchini Misri mara baada ya sheria mpya kuwekwa saini.

Mwezi uliopita mswada mwingine ulipitishwa na bunge la nchi hiyo lakini bado rais Sisi hajaupitisha unadai kuwa mtu yeyote ambaye ana marafiki zaidi ya 5,000 kwenye mtandao wa kijamii inabidi awe kwenye uangalizi maalum.

Nchi hiyo baada ya kufungia maandamano ,mitandao ya kijamii ilikuwa ni sehemu pekee ambayo wamisri walikuwa wanaweza kuikosoa serikali.

Mwezi uliopita Shiria la Human rights watch lilitoa angalizo mara baada ya mamlaka ya taifa hilo kuanza kuwafungulia kesi wanaharakati,waandishi wa habari na yeyote ambaye atayekosoa nchi hiyo .