Serikali yafanikiwa kuteketeza tani 50 ya dawa za kulevya


Mexico imeziharibu tani 50 za dawa Za kulevya ya Methamphetamine katika eneo ambalo dawa hizo zinatengenezwa.

Jeshi la Wanamaji la Mexico limesema eneo hilo limegunduliwa na wanajeshi wa kikosi hicho.

Ripoti za kijasusi zimeeleza kwamba tani za dawa za kulevya zilikuwa zinatengenezwa katika mji wa Alcoyonqui, katika maeneo ya milimani, yapata Kilomita 19 nje ya mji mkuu wa jimbo la Sinaloa.

Jimbo hilo ndilo lililokuwa eneo la kufanyia kazi la JOAQUIN GUZMAN maarufu "El Chapo" ambaye aliongoza kundi la uhalifu lililokuwa na nguvu hadi kukamatwa kwake mwaka juzi.

Kesi yake itasikilizwa nchini Marekani baadae mwaka huu.

Tangu kukamatwa kwa "El Chapo" makundi mengine ya kutengeneza dawa za kulevya katika jimbo la Sinaloa na sehemu nyingine za Mexico yameendel eza utengenezaji na uuzaji wa dawa hizo katika nchi za nje hasa Marekani.