Simba SC yatangaza kamati yake ya uchaguzi mkuu


Uongozi wa klabu ya Simba umeteua rasmi wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Kamati hiyo imeteuliwa kufuatia agizo la Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoka siku 75 kwa klabu hiyo pamoja na Yanga kwa ajili ya kufanya uchaguzu ili kuwapata viongozi wapya.

Wajumbe hao ni
Boniface Lyamwile - Mwenyekiti
Steven Ally - Makamu Mwenyekiti
Issa Batenga - Katibu
Idd Mbita - Mjumbe na
Richard Mwalwiba - Mjumbe

Kamati hiyo itatangaza tarehe ya uchaguzu hivi karibuni na kuitisha uchaguzi wa wajumbe wa bodi ya Simba Sports Club Company Limited  ambao watachaguliwa kwa mujibu wa ibara ya  27 ya katiba ya Simba SC Company Limited ya mwaka 2018.