Sirro alifumua jeshi la Polisi, RPC Mwanza ahamishwa


MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro,  amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza na mkoa wa Pwani.

Katika mabadiliko hayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi, (DCP), Ahmed Msangi amekuwa Mkuu wa Kitengo cha Makosa Dhidi ya Binadamu, Makao Makuu ya Upelelezi jijini Dar es salaam, huku nafasi yake ikichukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Jonathan Shana,  ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani.

Aidha, nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Wankyo Nyigesa ambaye alikuwa Mkuu wa Oparesheni Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imesema  mabadiliko hayo ni kawaida  ndani ya jeshi la Polisi.