8/10/2018

Snura anusurika kifo baada ya kupata ajali

MSANII wa Muziki wa Mduara Bongo, Snura Mushi amenusurika katika ajali ya gari mkoani Lindi alikokwenda kufanya shoo.

Ajali hiyo ya Snura aliyekuwa ameongozana na anayedaiwa kuwa mpenzi wake, Minu Calypto na madensa wake imetokea jana Alhamisi Agosti 9, 2018 wakati dereva wake akijaribu kukwepa korongo.

Minu Calypto ameandikwa; Jana mida ya saa nne usiku tulipata ajali mimi na Snura Mushi na ma-dancer wetu wawili pamoja na dereva… Gari ilipinduka ila tunashkuru Mungu tuko salama… #WeGood.

Kuna video ambayo sio nzuri (bad taste) ipo mtandaoni ikimuonyesha Snura Mushi akipatiwa matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye ajali hiyo.