Tanzania, Kenya, Zimbabwe kuoneshana ubabe mashindano ya mdahalo 'Mwalimu Nyerere'


Zaidi ya wanafunzi 200 kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wamekutana nchini Tanzania kwa ajili ya kushiriki katika mashindano ya mdahalo 'Mwalimu Nyerere' yanayofanyika katika Shule ya Seminari ya Al Mustazir Nslamic jijini Dar es Salaam.

Mdahalo huo umeandaliwa na Shule ya Al Mutanzir Islamic yenye lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi wa kujiamini, kuchanganua mada mbalimbali, kujenga hoja na kuzitetea pamoja na kufanya vizuri katika mithiani yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Shule ya Al Mustazir Beuben Kimani, amesema kuwa  madahalo huo utafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo.

Amesema kuwa katika mdahalo wanafunzi kutoka Shule mbalimbali  watashindana na Agosti I2 mwaka huu washindi watapewa zawadi.

Kimani ameeleza kuwa kuna wanafunzi zaidi ya nusu ya washiriki wametoka nchini mbalimbali Kenya, Zimbabwe, Zambia pamoja na Namibia.

"Kwa hapa Tanzania miongoni mwa shule zinazoshiriki ni Al Muntazir Islamic, Sabani Robert, Fedha Boys, Fedha Girls, Aghakhani, Tusime" amesema Kimani.

Kimani ameeleza kuwa shule ambazo zitafanya watapewa zawadi ili kutoa hamasha kwa washiriki zaidi.

Msimamizi wa mdahalo Shule ya Al Mutanzir Islamic Gertrude Mtenga, amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha shule yake inafanya vizuri.

Amesema kuwa mwaka huu wanafunzi wake watashika nafasi ya kwanza kutokana na elimu ya kutosha waliopewa.

"Mwaka wa jana hatukuweza kushika nafasi ya kwanza ila mwaka huu tutafanya vizuri kutokana wanafunzi wangu wamefanya maandalizi yakutosha" amesema Mtenga.

Amefafanua kuwa mdahalo kwa wanafunzi ni muhimu kwani inamsaidia kuwa katika hali ya kujiamini, kujifunza mambo mbalimbali kwa muda mfupi pamoja na kuwa na uwelewa wa kupanga hoja wakati wa kuzungumza.

Kwa upande wa wanafunzi wamejipanga vizuri katika kuhakikisha kila mtu anafanya vyema katika mashindano hayo.

Mwanafunzi wa Shule ya Al Mutanzir Islamic Husseina Nurbhai, amesema kuwa kutokana na maandalizi waliofanya kabla ya mdahalo huo wanaamini watafanya vizuri.

Nurbhai anasoma kitato cha nne mchapuo wa sayansi, ameeleza kuwa licha ya changamoto baadhi ya mada hasa katika uchumi  atajitaidi ili kuhakikisha Shule yake inakuwa mshindi wa kwanza.

Naye Saloha Aboud amesema kuwa amejipanga kushindana na shule nyingine katika mada mbalimbali ambazo anashiriki katika mdahalo.

"Kwa sasa nina uzoefu wa kutosha katika mashindano hayo kwani niliadha tangu nikiwa kidato cha pili, naamini nitafanya vizuri" amesema Aboud mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya seminari ya Al Mutanziri Isramic.