Aliyewapiga Yanga 'Hat Trick' atumiwa mpira wake na TFF


NYOTA wa Stand United, Alex Kitenge ambaye aligeuka mwiba mchungu kwa Yanga baada ya kuwafunga magoli matatu pekee yake 'Hat trick' amekabidhiwa mpira wake na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF.

Kitenge alifunga magoli matatu licha ya Timu yake kufungwa magoli 4-3 ambapo kwa kanuni za Ligi Kuu alipaswa kupewa mpira wake lakini TFF haikumpa kwa kisingizio cha kuwa na uhaba wa mipira.

Uongozi wa Stand United umethibitisha mchezaji wao kutumiwa mpira wake kupitia kwa maafisa wa TFF.