.

9/14/2018

Aslay aeleza mapenzi yalivyomtenda, "Wanawake wengine wanakupenda kwa kuwa msanii"


Unafahamu sababu ya Aslay kuamua kukaa bila ya kuwa na mpenzi?

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Ijumaa hii kuwa sababu ya kuamua kukaa singel ni kutokana na kuumizwa katika mapenzi na aliyekuwa ex wake ambaye hakumtaja jina japo alikataa kuwa ni mama watoto wake ambaye anafahamika kwa jina la Tessy.

"Nilishawahi kuumia kwenye mahusiano ya kimapenzi lakini mahusiano hayo hayakuwa kati yangu na mama mtoto wangu Tessy ni ya mwanamke mwingine, ndio maana kwa sasa nipo single,” amesema Aslay.

Pia msanii huyo ameongeza kuwa, "Sitaki kukurupuka kutafuta mahusino mapya kwa sababu wanawake wengine wanakupenda kwa kuwa ni msanii na wengine wana tamaa."