Hamisa Mobetto
Akizungumzia vigezo vya mwanaume anayemtaka, Hamisa amesema kuwa kwa sasa hapendi kuolewa na vijana na anatafuta Mzungu mwenye umri mkubwa kuanzia miaka 45.
“Mimi hapa nataka labda mzungu au mtu mzima, awe alishawaki kuachwa au Mgane kwa hiyo ndio hivyo, yaani nikisema kijana dah hapana. Awe angalau miaka 45 kwa sababu mimi mwenyewe nina watoto sasa ukisema kijana yeye mwenyewe bado anakua atawezaje kulea watoto wangu,“amesema Hamisa Mobetto kupitia EATV.
Hamisa Mobetto tayari ameshazaa watoto wawili na wanaume wawili tofauti tofauti, ambao ni Diamond Platnumz na Majizzo na amesema kwa sasa hawezi kurudiana na yeyote kati yao.
Kwa upande mwingine, Hamisa Mobetto amekiri kuwa sauti iliyosambaa mitandaoni wiki mbili zilizopita akiongea na Mganga wa kienyeji ilikuwa ni ya kwake.