Hukumu tatu zatolewa na Mahakama ya Afrika kwa Tanzania


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu imetoka Hukumu ya kesi Tatu zilizokuwa zinaikabili serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika Hukumu ya Shauri Namba 16/2016, malalamikaji ni Diocles Wiliam dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  akilalamikia mwenendo wa kesi iliyomhukumu jela miaka 30 jela  kwa Kumbuka Mtoto wa Umri wa miaka 12,

Baada ya Kusikiliza Shauri Hilo kwa Pande zote mbili,  mahakama ikabaini palikuwa na ukiukwaji wa Haki za mtuhumiwa wakati wa mwenendo wa Shauri Hilo hivyo kuamuru kurejelewa upya Shauri Hilo ndani ya kipindi cha miezi Sita, na kuhakikisha katika kipindi kisichozidi miaka miwili mahakamani iwe imetoa maamuzi.

Hukumu nyingine ni ya Shauri Namba 20/2016  lililofunguliwa na Anaclet Paul dhidi ya Serikali ya jamhuri  ya Muungano wa Tanzania , akipinga Hukumu ya miaka 30 na mwenendo wa kesi iliyomhukumu jela kwa kukutwa na hatia ya wizi wa kutumia silaha,
Katika Shauri Hilo mahakama imetupilia mbali Ombi kufutiwa kifungo hicho, huku ikiitaka serikali ya Tanzania  kumlipa Fidia ya shilingi Laki Tatu kutokana na kumnyima Haki ya msaada wa kisheria.

Hukumu Namba Tatu ni ya Shauri Namba 27/2016 la Minani Evarist dhidi ya Serikali ya Tanzania akiitaka mahakama kumwachia huku kutokana na kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia ya Kumbaka Binti wa miaka 15.

Mahakama imetupilia  mbali ombi la kuachiwa huru huku ikiitaka serikali kumlipa shilingi Laki 3, baada ya kubaini palikuwa na ukiukwaji wa Sheria kwa kumnyima mtuhumiwa Haki ya kupata msaada wa kisheria.