India yamwaga vifaa vya Bilioni 2 kwa Wizara ya Afya


Serikali ya India imetoa msaada wa dawa na vifaa tiba kwa serikali ya Tanzania wenye thamani ya shilingi bilioni mbili kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha upatikanaji dawa na huduma za afya nchini.

Msaada huo umekabidhiwa na balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya kwa bohari kuu ya dawa (MSD) jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambaye ameishukuru serikali ya India na kubainisha baadhi ya dawa zilizotolewa kuwa ni pamoja na dawa ya kuzuia wajawazito kuvuja damu baada ya kujifungua.