Mambo Matatu Ya Kukusaidia Kuboresha Kipato Chako Kwa Uhakika


Msingi wa kujenga kipato kikubwa na hatimae kuwa huru kifedha huwa haupatikani kwa bahati mbaya. Msingi huo zaidi unapatikana kwa wewe kujua zaidi mambo ya msingi yatakayoweza kukusaidia kuboresha kipato chako kila iitwapo leo.

Kwa kawaida kuna mambo ambayo ukiyajua yana msaada mkubwa sana katika kukusaidia kuweza kuboresha kipato chako. Mambo haya wengi tunayajua ila kwa sababu sisi ni binadamu tunakuwa tuna yasahau sana.

Kupitia makala haya nataka nikuonyeshe mambo ya msingi matatu, ambayo ukiyazingatia yatakusaidia sana kuweza kuboresha kipato chako karibu kila siku na maisha yako yakawa bora zaidi. Mambo hayo ni yapi? Karibu tujifunze.

Jambo la kwanza; angalia matumizi yako.
Ni wazi kabisa matumizi uliyonayo yanaweza kukusaidia kuboresha kipato chako au yakakiharibu kabisa. Kama matumizi yako ni mabaya kipato chako hakiwezi kuwa bora pia hata iweje, lazima utakuwa una kipato kibovu tu ambacho hakitakusaidia.

Hapa unaona, eneo mojawapo la kushughlika nalo sana kama unataka kuboresha kipato chako ni juu ya matumizi uliyonayo. Matumizi uliyonayo ukiweza kuyapangili a vizuri, itakusaidai kuweza kupiga hatua ya kukusaidia kuboresha kipato chako kwa kiasi kikubwa.

Jambo la pili; angalia uwekaji wako wa akiba.
Je, una weka akiba vya kutosha au unaweka akiba kama matone ya mvua kwa kurasha rasha au huweki akiba kabisa? naamini majibu hapa unayo wewe mwenyewe kipi ambacho unakifanya kwenye swala zima la uwekaji wa akiba.

Ukiweza kuboresha juu ya uwekeji wako wa akiba vizuri uwe na uhakika hata matumizi yako yatakuwa vizuri sana kiasi cha kwamba kuweza kuboresha kipato chako na kukusaidia hata kuweza kuwekeza kwenye miradi mingine.

Jambo la tatu; angalia jinsi unavyowekeza.
Najua unaweza ukawa kweli matumizi yako sasa yako sawa, na umeamua kuweka akiba je, kitu kingine unawekeza? Kama huwekezi unategemea kipato kimoja na pia hapo hapo ukategemea kipato ulichonacho kibadilike naomba hapo usahau.

Mafanikio makubwa ya kuweza kufikia ngazi ya kuongeza kipato chako na wewe hadi kufikia uhuru wa kifedha yanapatikana kutokana na wewe kuweza kuwekeza. Usipowekeza sahau mafanikio hayo.

Ni muhimu na msingi sana kuzingatia matumizi yako ya pesa, uwekaji wako wa akiba na kuwekeza pale unaotafuta kuboresha kipato chako kwenye maisha. Unapozingatia mambo hayo uwe na uhakika kipato chako lazima kitakuwa bora hata kama kwa sasa mambo yanaonekana mabaya.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.