.

9/14/2018

Mbowe uso kwa uso na Dkt. Bashiru Ally uchaguzi Ukonga


Wakati imebaki siku moja kuhitisha kampeni za uchaguzi mdogo wa marudio wa Wabunge na madiwani, chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kitaongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe ambapo ataongoza viongozi wengine.

Mbowe atambatana na viongozi waandamizi wa Chama wakiwemo Wajumbe wa Kamati Kuu, katika kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa marudio Jimbo la Ukonga.

Pia Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalim ataongoza viongozi wengine waandamizi wa chama wakiwemo Wajumbe wa Kamati Kuu kufunga kampeni Monduli huku Jonh Mnyika akiongoza kuhitimisha kampeni Kata ya Vingunguti. 

Aidha kwa upande wa chama cha Mapinduzi (CCM)katika kuhitimisha kampeni hizo katika jimbo la ukonga zitaongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Bashiru Ally.