.

9/14/2018

Mourinho athibitisha Luke Shaw na atacheza dhidi ya Watford Jumamosi


 Jose Mourinho ambaye ni Kocha wa Manchester United amethibitisha kuwa beki wa kushoto wa timu hiyo Luke Shaw anauwezekano mkubwa wa kucheza mchezo wa Siku ya Jumamosi dhidi ya Watford katika Uwanja wa Vicourage road baada ya beki huyo kuumia wakati anatimiza wajibu wake kwenye timu ya taifa katika michezo ya kimataifa mwishoni mwa wiki.

Kulikuwa na wasiwasi mkubwa sana kama Shaw hataweza kurejea uwanjani mapema kufuatia kuumia kichwa katika mgongano na beki wa Uhispania Dani Carvajal katika Uwanja wa Wembley ingawa England walipoteza katika michezo hiyo ya kimataifa kwa goli 2-1 nymbani lakini mlinzi huyo aliweza kutoa msaada wa goli kwa Rashford.

Mourinho alibainisha kuwa daktari wa klabu amethibitisha upatikanaji wa Shaw kutokana na matibabu, lakini aliongeza kuwa hajaamua kama ataweza kumruhusu kucheza dhidi ya Watford Jumamosi.”Sijui kama atacheza” ,” Mourinho alisema. “Bado tuko naye kwenye mazoezi”. “Kinyume na habari zingine, kwa mtazamo wa protocol na kulingana na daktari wetu Shaw atakuwa huru kucheza.””Hali tunayoweza kuiweka wazi ni kwamba kama tutamchezesha mchezaji ambayo hakuwa na mafunzo na timu wiki nzima wakati wa maandilizi, au ikiwa, ndo hivyo, tunaamua tu kumchezeshaa.”

Baada ya kujitahidi katika changamoto nyingi katika msimu uliopita , Shaw amefanya kazi kubwa sana kwa kuanza kwa nguvu katika kampeni za kusaka namba msimu huu 2018-19, akicheza kila dakika ya michezo yao ya kufungua yote minne.Mourinho pia alitoa taarifa juu ya kikosi chake chote kabla ya safari ya kuelekea Watford,ambapo Mourinho alisema ” kuna mashaka makubwa kama Marouane Fellaini atacheza .Ander Herrera atakuwa nje.kwani alikuwa na shida moja kidogo katika kifundo kwani aliumia katika mafunzo ndani ya hii wiki hivyo pia ni shaka,” Mourinho aliongeza.

“Diogo Dalot na Marcos Rojo watacheza usiku wa leo katika mchezo wa timu ya Manchester chini ya miaka 23. Kama watacheza dakika 90 basi tunatarajia itakuwa mwisho wa mchakato wao na kurejea na kuwa tayari kuungana nasi wiki ijayo kwa ushindani kamili.”