Mtatiro awachana Chadema kuwa ni matapeli

Julius Mtatiro afunguka mazito kuhusu Chadema na kusema kuwa alihama upinzani kwa sababu Chadema ni Chama cha matapeli.

Mtatiro ametoa kauli hiyo jana Alhamisi katika mkutano wa kampeni za CCM jimbo la Ukonga. Katika mkutano huo, Mtatiro amesema ameshtuka mchezo mchafu ulioko Chadema na kwamba wapo kimaslahi.

"Tupo hapa kumsapoti Mwita Waitara, ukiona kiongozi kama mimi niliyekaa miaka kumi  na nimeachana na utapeli wewe kijana shtuka kapige kura kwa Waitara," amesema.

Mtatiro ambaye chama chake cha zamani cha CUF kilikuwa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) unaoundwa na vyama vinne vya NLD, Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF.