.

9/14/2018

Mwadui FC waipunguza kasi Azam kwenye ligi kuu


Ligi ku ya Tanzania Bara imeendelea tena Ijumaa hii baada ya kusimama kwa takribani  wiki mbili kupisha mchezo wa timu ya Taifa Stars.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa majira ya mchana katika uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga uliwakutanisha Mwadui FC na Azam.

Mchezo huo umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana goli 1-1.

Azam ndio walikuwa wakwanza kupata goli lao kupitia kwa Abubari Salum maarufu Sure Boy kwenye dakika ya 55 ya mchezo huo, hata hivyo Mwadui walisawazisha dakika ya 71 kupitia kwa mchezaji wao Edwin Innocent.