Mwanasiasa wa Upinzani ajiengua katika chama chake

Mwanasiasa mkongwe na mashuhuri wa upinzani nchini Burundi, Agathon Rwasa amejiengua katika muungano wa vyama vya upinzani nchini humo na yumo mbioni kusajili chama kipya cha siasa.

Katika mkutano na wafuasi wake wasiopungua 500 kutoka mikoani ,wamewakilisha mapendekezo mbalimbali kwa mujbu wa sheria ili wafikishe maombi yao kwenye wizara ya mambo ya ndani kwa usajili wa chama chao cha National Liberty Front Amizero y'Abarundi.

Rwasa amesema itawalazimu wanasiasa wa upinzani kujidhatiti katika vyama vyao ili baadae kujiweka pamoja wakati wa mpambano wa uchaguzi kwa mujibu wa katiba mpya.

Nkurunziza asema ataachia madaraka 2020 Burundi
Wapiga kura waidhinisha marekebisho ya katiba Burundi
Pia amewataka wafuasi wake kuwa watulivu,wavumilivu na kuchangia kwa hali na mali toka sasa hivi hadi itapofikia uchaguzi mkuu miaka miwili ijayo.

Kwasasa Rwasa ni Makamu Spika wa Bunge akiwakilisha mseto wa vyama vya upinzani wa amizero y'abarundi.

Muungano huo katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2015 ulishika nafasi ya pili ukitanguliwa na chama tawala CNDD FDD cha Rais Pierre Mkurunziza.