Real Madrid hawataki kucheza Marekani

Baada ya uongozi wa LaLiga wiki kadhaa zilizopita kutangaza mpango maalum wa kuitangaza zaidi Ligi Kuu Hispania nje ya mipaka ya Hispania, moja kati ya mpango wao huo umeanza kupata vikwazo kutoka katika vilabu wanachama.

Uongozi wa LaLiga ulitangaza kuwa moja kati ya mpango wake wa kuikuza na kuongezea thamani Ligi hiyo, wataruhusu baadhi ya game za LaLiga zikachezwe nchini Marekani ili kuiongezea umaarufu na thamani zaidi Ligi hiyo.

Baada ya taarifa hizo kutoka Rais wa club ya Real Madrid Florentina Perez ameamua kuweka wazi msimamo wake, kuwa kama watacheza LaLiga nchini Marekani ni sawa kwa vilabu vingine lakini sio kwa club yake ya Real Madrid.