Ujenzi wa bweni washusha takwimu za mimba Shule ya Sekondari


Na Timothy Itembe, Tarime

Takwimu za mimba kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Bwiregi zimeshuka baada ya Mfuko wa dhamana ya jamii ya North Mara kujenda bweni la wasichana kwa lengo la kulala na kujisomea hapo shuleni pamoja na kuongeza ufaulu.

Mkuu wa shule ya sekondari Bwiregi, Josephat Bwenye alisema kuwa kabla ya kupata mradi wa hosteli shuleni hapo kutoka kwa  mfuko wa dhamana wa jamii ya North Mara(Trust Fund) mimba mashuleni katika shule hiyo kiwango kilikuwa wasichana 05 kwa mwaka lakini baada ya kujengewa bweni kiwango hicho kimeshuka kutoka wasichana watano hadi kufikia msichana mmoja kwa mwaka.

“Mradi tuliopata wa kujengwewa bweni la wasichana kutoka mfuko wa dhamana ya ya jamii  ya North Mara umepunguza mimba katika shule yetu kutoa wasichana watano kwa mwaka hadi kufikia msichana mmoja kwa mwaka hii ni kutokana na wasichana kulala shuleni ambapo wasichana wengi wameepukana na vishawishi vya wanaume njiani walivyokuwa wanakumbana navyo vya wanaume,” alisema Bwenye.

Bwenye aliongeza kuwa mfuko huo umejenga bweni la kulala wasichana wapatao 48 lakini kwasasa wasichana wanaolala shuleni hapo  ni 43  hii ni kutokana na uhiari wao unaotokana na wazazi kuwakubalia kuchagia garama za chakula pamoja na magodoro.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mfuko wa Dhamana ya Jamii ya North Mara,Rhobini Matenga alisema kuwa mradi huo ni moja ya miradi ambayo inaibuliwa na jamii ambapo katika shule hiyo Trus Fund wamejenga hostel moja,Choo bora cha kisasa kwa wanafunzi wa hosteli na kujenga eneo la kufulia na kuogea ndani ya choo hicho ya pamoja na kuwajengea shule hiyo matenki ya kuvunia maji ambayo yana uwezo wa kuvuna maji lita 8,000 pindi mvua inaponyesha.

Shule hii haikuwa na maji lakini walipoleta maombi ya kuchimbiwa kisima bodi ilipitisha na kuwajengea matenki mawili ya maji ambapo moja lina uwezo wa kuvunia maji zaidi ya lita 500 na linguine lina uwezo wa kuvuna maji lita 300 jumla lita 8,000 na kuwaondolea wanafunzi kutembe mwendo mrefu wakienda kutafuta maji mtoni umbali wa kilomita zaidi ya mbili.

Juma Elias Kegoye moja wa mfuko wa dhamana ya jamii ya North Mara alisema kuwa wanasaidia jamii baada ya kuibua miradi na kuleta maombi ndani ya mfuko huo kwasbabu ndio kazi yao kutekeleza miradi na maendeleo kwa jamii ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha mapinduzi.

Awali alipotembelea Rais wa jamuhuri ya muungano ya Tanzania,John Pombe Magufuli alipokea kilio cha Maji kutoka kwa wananchi wa Wilaya Tarime ambapo ni kilio cha mda mrefu.