Uturuki yaunga mkono mkutano kati ya Korea Kaskazini na Kusni.


Uturuki imeunga mkono mkutano wa tatu kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusni.

Rais wa Korea Kusini na Korea Kaskazini wamefanya mazungumzo mjini Pyongyang kuanzia 18-20 Septemba.

Moon Jae In amemshawishi Kim Jong Un kuachana na makombora ya nyuklia.

Uturuki inatumai kuwa mazungumzo hayo yatasaidia kuleta amani ya kudumu nchini Korea.

Katika siku ya pili ya mkutano,Kim aliahidi kuachana kabisa na silaha za nyuklia baada ya kuzungumza na Moon.

Kulingana na shirika la habari la Yonhap la Korea Kusini,,viongozi hao wawili pia wamesaini mkataba wa kijeshi kuhakikisha kuwa migogoro inapungua

Kim Jong Un na Moon Jae In pia wamezungumzia jinsi ya kuunganisha reli na barabara kati ya mataifa hayo mawili,kuandaa kwa pamoja mashindano ya olimpiki 2032 na kuanzisha kituo kipya cha kukutanisha familia.