Watanzania wanaoishi nje wamponza Msemaji wa Chadema


INAELEZWA kuwa kushikiliwa kwa Msemaji wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Tumaini Makene kumesababishwa na watanzania wanaoishi nje ya (Diaspora) ambao wanatumia blog ya chama hicho bila kusajiliwa.

Makene alikamatwa na Jeshi la Polisi mapema wiki hii akidaiwa kuendesha blog hiyo na hadi leo anashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya uchunguzi wa kujua maudhui ya blog hiyo iitwayo Chadema.blogspot.com ambayo haina usajili kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA.

Wakili wa Makene, Fred Kihwelo amesema msemaji huyo ni kama ameponzwa na diaspora hao huku akisema bado wanafuatilia dhamana au kuangalia uwezekano wa kupelekwa mahakamani.

" Makene hahusiki na uendeshaji wa hii blog ambayo inatajwa, hakuna sehemu yoyote jina lake linaonekana, diaspora ambao ni wanachama wa Chadema ndio wanaoiendesha," amesema Wakili Kihwelo.