Zaidi ya milioni 170 zachagwa leo ajali Mv Nyerere kusaidia walioathirika


Mpaka kufikia saa 12:00 jioni ya leo tarehe 22 Septemba 2018, jumla ya Sh. Mil 180 zimechangwa kwa ajili ya kusaidia walioathirika kwenye ajali ya MV. Nyerere

Wadau waliotoa michango hiyo mpaka sasa ni Vodacom (Mil 10), Tigo (Mil 150), Azim Dewji (Mil 10) na Waislam jamii ya Shia (Mil 10).

Pia michango mingine imeendelea kutolewa ikiwa ni pamoja na katoni za maji zaidi ya 6,000.

Serikali leo imefungua akaunti maalum kwa ajili ya kuchangia waathirika hao. Akaunti hiyo ni ‘Maafa ya MV Nyerere 31110057246 Tawi la MNB Kenyatta, Mwanza.’

Wadau hao wametoa michango hiyo leo katika Kisiwa cha Ukara ambapo ajali hiyo ilitokea Septemba 20, Mwaka huu.

Jenister Muhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu akizungumza katika Kisiwa cha Ukara amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa waathirika.