Australia yaonywa na Jumuiya za nchi za kiislamu (OIC)

Jumuia ya ushirikiano wa nchi za kiislamu (OIC) siku ya  jumanne imetoa onyo kwa nchi ya Australia kwa matokeo mabaya yatakayotokea kutokana na Australia kuhamishia ubalozi wake nchini Izrael kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.

Katika maelezo yaliyotolewa na umoja huo ambao makao makuu yake yapo Jeddah, imeambia Canberra isichukue hatua hiyo ambayo ni uvunjifu wa sheria za kimataifa pamoja na maamuzi ya umoja wa mataifa.

Katibu mkuu wa OIC Yousef bin Ahmed Al-Othaimeen alisema Jerusalem ni sehemu ya Palestina ambayo imekaliwa kimabavu na Izrael tangu mwaka 1967.

" OIC inapinga tendo au jaribio lolote  linajaribu kubadilisha hadhi ya kisheria ya ya mji unaokaliwa kimabavu wa Jerusalem" alisema katika maelezo yake.

Aliendelea kwa kuiambia Australia iunge mkono suluhisho la kuwapo mataifa mawili ili kulinda amani na usalama wa eno hilo na dunia kwa ujumla.

Waziri mkuu wa Australia Scott Morrison alisema Australia ipo tayari kuhamisha ubalozi wao kutoka Tel Aviv kuupeleka Jerusalem na kuitambua Jerusalem kama makao makuuya Izrael.

Jerusalem imeendelea kuwa kitovu cha mgogoro wa mashariki ya kati.Wapalestina wanategemea kwamba Jerusalem mashariki eneo linalokaliwa kimabavu na Izrael tangu mwaka 1967 inaweza kuwa makao makao makuu ya taifa la Palestina huru.