10/13/2018

BREAKING NEWS: Pengo Jingine Chadema, Mbunge ang'atua atua CCM


Mbunge wa jimbo la Babati mjini Pauline Philipo Gekul, amejiuzuru nafasi yake ya ubunge ambapo amefika maombi yake ya kujiuzuru wadhifa huo kwa spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Job Ndugai, ambapo amesisitiza kuwa amefanya kazi kwa miaka nane katika kuwatumikia wananchi.

Mbenge huyo wa babati mjini, amesema kuwa katika kipindi chote cha miaka nane ambacho amefanya kazi akiwa chini ya chama cha demekrasia na maendeleo chadema amedai kuwa amekutana na changamoto nyingi ikiwemo kutelekezwa tangu uchaguzi ulipoisha wa mwaka 2105.

Vilevile amedai kuwa katika kukamilisha ahadi ambazo alikuwa amewapa wakazi wa babati mjinilikuwa akishirikiana na viongozi wa CCM katika kukamilisha ahadi hizo ambazo aliweka katika jimbo lake hilo.

Kufuatia hayo Mbunge Pauline ametangaza kujiunga na CCM ili kukamilisha miradi mingine ikiwemo miradi ya maji katika vijiji na mitaa ya Babati, Vilevile kukamilisha mradi wa Barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 10.