BREAKING: Pigo lingine latua Chadema, Mbunge mwingine akimbilia CCM


Mbunge wa Jimbo la Simanjiro kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, James Ole Millya ametangaza rasmi leo kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani ikiwemo ubunge na kuomba kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM.

Millya ambaye alijiunga na Chadema miaka sita iliyopita akitokea CCM amekuwa mbunge wa nne kutoka chama hicho kuondoka na kujiunga na CCM huku naye akisema ameamua kujizulu kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Rais Dk John Magufuli katika kuwatumikia wananchi.

Millya amemuandikia Spika wa Bunge, Job Ndugai barua ya kuthibitisha kujiuzulu ubunge huo.