Chadema Babati hali mbaya, Diwani mwingine awakimbia


Na John Walter-Babati
Baada ya mbunge wa Chadema jimbo la Babati mjini Paulina Gekul  kujiunga na Chama cha Mapinduzi siku mbili zilizopita, hatimaye diwani wake kutoka kata ya Maisaka amemfuata.

Diwani huyo aliyekuwa na msimamo katika vikao vya Maamuzi, Abrahamani Kololi amejiunga na CCM Leo oktoba 16.2018  katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Manyara Alexender Mnyeti uliofanyika katika mtaa wa Sinai kata ya Maisaka na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa na serikali.